Nchini Rwanda, Kigali imetangaza kuanza msako mkali na kuweka gerezani walemavu wote wanaojihusisha na vitendo vya kuomba barabarani, kwa madai kuwa ni chanzo cha uchafu wa jiji na imesema kama hawataacha kuomba omba watakabiliwa na kifungo.
Msako huo unaweza kutekelezwa wakati wowote kuanzia sasa, hivyo umewaonya walemavu hao na kuwasihi kuacha na endapo hawataacha kuomba omba watakabiliwa na kifungo hiko.
Baadhi ya wananchi wamepinga uamuzi huo wakisema, unalenga kukandamiza walemavu na watu masikini ambapo mashirika ya kiraia nchini Rwanda yameshauri kwamba kabla ya utekelezaji wa msako huo yafanyike mazungumzo ya pande zote.
Ripoti mbalimbali zimekuwa zikiitaja Kigali kuwa ni miongo mwa majiji masafi barani Afrika huku ripoti nyingine hususani zile za kutetea haki za binadamu zikiishutumu serikali hiyo kwa kuwafunga watu wasiojiweza.