Licha ya kuwa Mkurugenzi wa ‘Creative’ katika Kampuni ya GSM, Msanii wa Nyimbo za Kizazi Kipya nchini Tanzania, Omary Nyembo maarufu Ommy Dimpoz amesema kuwa hatoweza kuwa shabiki wa Young Africans katika maisha yake.

Ommy Dimpoz ambaye ni shabiki wa Simba SC, amesema hayo katika zoezi la kutambulisha Jezi mpya za Klabu hiyo ya Wananchi jijini Dar es Salaam, Ommy amesema kuwa awali alipata dili la kuwa Balozi wa Kampuni ya GSM baadae alipewa ofa ya kuwa Mkurugenzi wa ‘Creative’ wa Kampuni hiyo.

“Awali nilipewa dili la kuwa Balozi wa GSM, lakini baadae baada ya kazi nzuri, Wakuu wa Kampuni walinipa ofa ya kuwa Mkurugenzi wa ‘Creative’ kutokana na kazi yangu. Baadae nilitakiwa kuajili vijana wenzangu ambao ni wabunifu”, amesema Ommy Dimpoz.

Dimpoz amesema alibahatika kuwapa madili Wasanii wenzake kama kina Marioo na Mavokali kutunga na kutoa nyimbo mbalimbali za Klabu hiyo kama sehemu ya kuburudisha mashabiki wake.

“Nakumbuka nilimuona Bosi akicheza wimbo wa ‘Bear Tamu’, nilimwambia Marioo ambaye ni mtunzi wa wimbo huo, nilimwambia kuwa atunge wimbo kwa kutimia ‘Melody’ ya wimbo huo kuhusisha na Yanga, na baadae alitoa wimbo wa ‘Yanga Tamu’, nilimsikilizisha Bosi na aliupenda wimbo huo”, ameeleza Ommy Dimpoz.

Robertinho: Ninarudi kuendelea na kazi
Young Africans yafungua ukurasa mpya