Mabingwa wa Soka Tanzania Bara na Wawakilishi wa nchi kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika Young Africans, wamezindua Jezi mpya sambamba na kusaini mkataba na Kampuni ya vifaa vya Kieletroniki ya Haier.

Young Africans imefanikisha mpango huo ikiwa ni sehemu ya kushiriki Michuano ya Kombe la Shirikisho Hatua ya Makundi itakayoanza rasmi Februari 12.

Mkataba kati ya Klabu hiyo na Kampuni ya Haier ambayo itakuwa Mdhamini Mkuu kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika Hatua ya Makundi una thamani ya Shilingi Bilioni 1.5

Young Africans itavaa Jezi zenye jina la wadhamini hao, katika mashindano ya kimataifa kwa msimu huu pekee (Kombe la Shirikisho Barani Afrika).

Katika hatua nyingine Young Africans imezindua Jezi mpya tatu (Nyumbani, Ugenini na chaguo la tatu), ambazo rasmi zitatumika kwenye Michuano ya Kimataifa.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi Februari 12, itaanza kampeni ya kucheza hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho kwa kucheza ugenini nchini Tunisia dhidi ya US Monastir.

Kabla ya kuondoka Tanzania, Young Africans bado itacheza mchezo wa mzunguuko wa 23 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo FC.

Ommy Dimpoz: Sitaisaliti Simba SC
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 31, 2023