Serikali, imeongeza bajeti katika Sekta ya Uvuvi hadi kufikia Shilingi 60 bilioni zitakazotumika katika ununuzi wa boti kama sehemu ya jitihada za kuimarisha mazingira ya kufaidika na fursa za soko la samaki za mabondo la nchini China.
Hayo yamebainishwa hii leo Novemba 11, 2022 Ikulu Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba na kuongeza kuwa, katika fedha hizo, zaidi ya boti 240 zitanunuliwa na kutolewa kwa vikundi vya wavuvi wanaovua kwa kutumia zana za kale.
Amesema, “Mradi huo wa kuongeza zana za kisasa ni programu ya miaka mitatu ya kushughulika na sekta za uzalishaji, kama mwaka huu zitanunuliwa boti 200, mwaka ujao wa fedha zitanunuliwa 300 na kuongezeka tena mwaka mwingine wa fedha unaofuata.”
Kuhusu zao na biashara ya Parachichi, Mwigulu amesema zipo hatua zilizochukuliwa za kuanzia mbegu bora za kisasa, zitakazohakikisha mazao hayo yanakuwa ya viwango vinavyotakiwa nchini humo.