Msafara wa kikosi cha Young Africans unatarajia kulutaondoka leo usiku kwenda nchini Nigeria kwa ajili ya kucheza mchezo wa klabu bingwa mkondo wa pili dhidi ya Rivers United,
Mchezo huo utachezwa jumapili September 19 kuanzia majira ya saa 12:00 jioni kwenye dimba la Adokiye Amiesimaka, Port Harcourt.
Young Africans inatarajia kuondoka na ndege ya kukodi na jumla ya watu 100 ikiwa ni Wachezaji, Viongozi wa bechi la Ufundi, Viongozi wa timu na mashabiki. wachezaji 22 ambao wanatarajia kuondoka na timu leo usiku kwenda mjini Port Harcourt upande wa Magolikipa Djigui Diarra, Eric Johora na Ramadhani Kabwili
Mabeki: Kibwana Shomary, Paul Godfrey, Adeyun Saleh, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Yannick Bangala na Abdalah Shaibu Ninja
Viungo: Mukoko Tonombe, Feisal Salum Fei Toto, Zawadi Mauya na Saido Ntibazonkiza.
Winga: Deusi Kaseke, Ditram Nchimbi, Jesus Moloko, Dickson Ambundo na Farid Mussa
Washambuliaji: Yacouba Songne, Heritier Makambo na Yusuph Athuman