Mazishi ya Malkia Elizabeth II, yatafanyika Septemba 19, 2022 huko Westminster Abbey, ambayo yanatarajiwa kuwa na mkusanyiko mkubwa zaidi ya wafalme na wanasiasa walioandaliwa nchini Uingereza kwa miongo kadhaa.

Shughuli hiyo ya mazishi, itafanyika katika ukumbi wenye uwezo wa kuchukua watu 2,000, kwa kuwajumuisha Familia ya Kifalme, viongozi wa ulimwengu, wanasiasa, watu mashuhuri, wafalme wa Uropa na wale wafanyakazi wa karibu na Malkia.

Inaarifiwa kuwa, mialiko tayari imetumwa kwa wakuu wa serikali na watu mashuhuri zaidi ya 500 mbali na washiriki wa familia za kifalme kote barani Ulaya, ambao wanaotarajiwa kuhudhuria hafla hiyo akiwemo Mfalme Philippe wa Ubelgiji, na Malkia Mathilde.

Uombolezaji wa kifo cha Malkia Elizabeth wa II. Picha na Africanews.

Mfalme Willem-Alexander wa Uholanzi, na mkewe Malkia Maxima na mama yake, malkia wa zamani wa Uholanzi Princess Beatrix pia wanatarajiwa kuwepo huku Ikulu ya Marekani ikithibitisha kuwa Rais Joe Biden atahudhuria pamoja na Mke wa Rais Jill Biden.

Mbali na washiriki wa familia za kifalme, toka barani Ulaya wanaotarajiwa kuhudhuria hafla hiyo, tayari Mfalme Philippe wa Ubelgiji na Malkia Mathilde wamethibitisha kuwepo.

Malkia Elizabeth II, alifariki dunia Septemba 8 2022 akiwa na miaka 96, akitajwa kama kiongozi aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi nchini Uingereza kwa kuwa madarakani kwa miaka 70.

Haji Manara apunguziwa adhabu TFF
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 15, 2022