Malkia Elizabeth wa Uingereza amekutwa na maambukizi ya virusi vya corona hii leo. Kasri la Buckingham limesema, Malkia ana dalili za kawaida kama za mafua.

Kasri hilo limesema kwamba kiongozi huyo mwenye miaka 95 ataendelea kufanya shughuli zake nyepesi katika Kasri la Windsor katika kipindi cha wiki chache zijazo na ataendelea kutibiwa na kufuata miongozo yote ya kupambana na maambukizi vya virusi vya corona.

Malkia Elizabeth tayari amepata chanjo tatu dhidi ya COVID.

Viongozi mbalimbali wamemtakia afya njema, ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu Boris Johnson, ambaye serikali yake wiki ijayo itaondoa vizuizi vyote vilivyosalia vya kupambana na maambukizi katika mkakati wake wa “kuishi na virusi vya corona” pamoja na kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour, Keir Starmer.

Imeelezwa kuwa watu kadhaa amepima virusi vya covid 19, Windsor Castle ambako Malkia Elizabeth anaishi.

Akamatwa kwa kuoa wanawake 17
Watoto 7 wauwawa kwenye Shambulio la anga Niger