Padri wa Kanisa Katoliki amepigwa risasi na kufa papo hapo eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo.

Vyanzo vya habari kutoka Kaskazini mwa jimbo la Kivu vimesema kuwa Padri, Étienne Nsengiunva alikuwa akikomnisha waumini Kanisani ghafla alijitokeza mtu mwenye silaha kanisani humo na kumfyatulia risasi.

Aidha, Tukio hilo limetokea wakati wa sherehe za ibada ya ubatizo wa wakristo wapya na wanandoa wapya ambazo zilikuwa zikiendelea.

Hata hivyo, taarifa zimesema kuwa muuaji huyo ametoka katika kundi la waasi wa Mai Mai Nyatura ambalo ni miongoni mwa vikundi vinavyopambana kudhibiti jimbo hilo lenye rasilimali za madini lakini pia uporaji wa fedha kutoka kwa wanavijiji.

 

 

JPM aahidi kutowaangusha viongozi wa dini
Video: Magufuli atumia mistari ya Biblia kusisitiza amani, Askofu Shoo atuma tena ujumbe mzito