Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa kamwe serikali yake haitawaangusha viongozi wa dini.

Ameyasema hayo Jijini Arusha katika Ibada ya kusimikwa kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Arusha, Isack Aman iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu.

Akizungumza katika Ibada hiyo, Rais Dkt. Magufuli ameyataka madhehebu yote kutambua kuwa serikali yake iko pamoja nao.

“Natambua kuwa serikali haina dini, viongozi wake waliomo ndio wana dini, kwa hiyo nawahakikishia kuwa natambua mchango mnaoutoa kama kiongozi wenu, sitawaangusha nipo pamoja nanyi,”amesema JPM

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Umoja wa Mapadri, Jimbo Kuu la Arusha, Padri Aloyce Kitomari amemuomba rais Dkt. Magufuli kuhamishwa kwa shule ya Msingi Nauri iliyopo jirani na Kanisa pamoja na kituo cha Polisi kitengo cha Usalama Barabarani.

Kakobe: Sitikisiki, Siyumbishwi...
Padri auawa kwa kupigwa risasi Kanisani