Klabu ya Azam FC imepiga panga kwenye kikosi chake kwa kuwaacha wachezaji wanne wa kimataifa.
Wachezaji hao ni Azam FC Obrey Chirwa (Zambia) na Mpiana Mozinzi (DR Congo), kiungo Ally Niyonzima (Rwanda) na Beki Yakubu Mohammed (Ghana).
Baada ya kuachana na wachezaji hao Azam FC mpaka sasa imekamilisha usajili wa wachezaji wanne wa kimataifa ambao ni Charles Zulu (Zambia), Rodgers Kola (Zambia), Paul Katema (Zambia) na Kenneth Muguna (Kenya).
Pia Azam inaendelea na mazungumzo ya kuvunja mkataba na kiungo Never Tegere (Zimbabwe) wenye uhakika wa kubaki msimu ujao ni Nico Wadada (Uganda), Bruce Kangwa (Zimbabwe), Daniel Amoah (Ghana), Mathias Kingonya (Uganda) na Prince Dube (Zimbabwe).