Mkuu wa kanisa Katoliki Duniani Papa Francis (86), amefanyiwa upasuaji wa tumbo katika hospitali ya Gemelli ya Roma.
Taarifa ya Vatican imesema, timu yake ya matibabu imeamua kwamba upasuaji ufanyike kwani ulihitajika kutokana na tatzilo alilonalo na kwamba anatarajiwa kukaa hospitalini kwa siku kadhaa ili kupata nafuu.
Papa Francis, alitakiwa kupelekwa hospitali baada ya mkutano wake wa kila wiki huko Vatican siku ya Jumatano asubuhi Juni 7, 2023, bila kutaja chochote kuhusu operesheni iliyopangwa.
Hata hivyo, inaarifiwa kuwa Papa alitumia dakika 40 kuchunguzwa katika hospitali ya Gemelli siku ya Jumanne Juni 6, 2023 na hali yake bado haijawekwa wazi juu ya operesheni hiyo.