Wizara ya Mambo ya ndani nchini Burundi, imesitisha shughuli za chama kikuu cha upinzani katika nchi hiyo kutokana na kasoro ambazo wakosoaji wanasema ni jaribio la kuwakandamiza wapinzani kuelekea uchaguzi wa wabunge mwaka 2025.

Hatua hiyo, iliyotangazwa mapema wiki hii inatajwa kuhatarisha au kupelekea kuzuka kwa machafuko ya kisiasa ambayo yameyakumba mataifa masikini ya Maziwa Makuu, katika miaka ya hivi karibuni.

Aidha, Chama cha National Freedom Council – CNL, kimelaani ukiukaji mkubwa wa katiba katika jaribio la kuvuruga na kudhoofisha chama baada ya hatua ya karibuni ya kuchorwa upya mipaka ya wilaya katika uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2025.

Hata hivyo, Wizara hiyo imesema itayajibu malalamiko ya viongozi wanane wa CNL walioondolewa madarakani, baada ya kumpinga rais wa chama hicho, Agathon Rwasa katika mikutano miwili ya chama hicho hivi karibuni.

Eneo la Shakahola kuwa Makumbusho - Serikali
Papa Francis alazwa, afanyiwa upasuaji wa tumbo