Wavuvi na Mkuu wa kundi linalowapinga wanamgambo wa itikadi kali za kislamu wamesema Wapiganaji wa Boko Haram wamewateka wafugaji 30 wa kabila la Fulani, karibu na Ziwa Chad kaskazini mashariki mwa Nigeria, wakidai fidia ili waweze kuwaachilia.

Wanamgambo hao, wakiwa katika boti nane walivamia vijiji vya wavuvi na wafugaji huko Tudun Kwastan, Kwatar Turare na Kwatar Kuwait katika mwambao wa ziwa hilo siku ya Ijumaa Juni 2, 2023 na kuwateka wafugaji hao wakiwemo wanaume na wanawake.

Mmoja wa wavuvi wa eneo hilo, Labo Sani amesema Wapiganaji wa Boko Haram wanadaiwa kuwa walikuwa wakichagua nyumba za kabila la Fulani katika vijiji hivyo na kuwachukua wanaume na wanawake, , mvuvi kutoka eneo jirani la Doron Baga, aliliambia shirika la habari la AFP.

Aidha, amesema Wanamgambo hao Waliacha ujumbe wakizitaka familia za mateka hao kuchangisha naira milioni 20 sawa na dola 43,000 kwa ajili ya kuachiliwa wapendwa wao.

Kiswahili: BAKITA yairudisha darasani nchi ya Malawi
Waanzisha vurugu kupinga ongezeko kodi ya mafuta