Kwa mara ya kwanza Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Senegal Pape Ousamn Sakho ametajwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya nchi hiyo, tangu alipojiunga na Simba SC ya Tanzania mwanzoni mwa msimu uliopita.
Kocha Mkuu wa Senegal Khalou Cisse amemtaja kiungo huyo katika kikosi chake ambacho mwishoni mwa juma lijalo kitaendelea na mchakato wa kusaka nafasi ya kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ kwa kuikabili timu ya taifa ya Msumbiji.
Sakho anaungana na wachezji wengine wanaocheza katika nafasi za Ushambuliaji walioitwa katika kikosi cha Senegal kama Nahodha Sadio Mane ( FC Bayern Munich), Boulaye Dia (Salerntana), Habib Diallo (Strasbourg), Bamba Dieng (Lorient), Iliman Ndiaye (Sheffield Utd) na Pape Ousmane Sakho (Simba SC).
Wachezaji wengine waliotajwa kwenye kikosi cha Senegal upande wa Walinda Lango: Seny Dieng (Opr), Alfred Gomis (Como) na Mory Diaw (Clermont)
Mabeki: Youssouf Sabaly (Betis Seville), Noah Fadiga (Brest), Kalidou Koulibaly (Chelsea), Formose Mendy (Amiens), Abdoulaye Seck (Maccabi), Moussa Niakhate (Nottingham), Ismail Jakobs (Monaco) na Abdallah Ndour (Sochaux)
Viungo: Gana Gueye (Everton), Nampalys Mendy (Leicester), Pape Gueye (Seville), Pathe Ciss (Vallecano), Pape Matar Sarr (Tottenham) Na Dion Lopy (Reims)
Senegal itacheza dhidi ya Msumbiji mjini Dakar katika Uwanja wa Diamniadio Olympic Machi 24, kisha itacheza ugenini mjini Maputo katika Uwanja wa do Zimpeto, Machi 28.
Senegal inaongoza msimamo wa Kundi L ikiwa na alama 06, ikifuatiwa na Msumbiji yenye alama 04, Rwandsa ipo nafasi ya tatu ikiwa na alama 01 na Benin inaburuza mkia ikiwa imepoteza michezo yote hadi sasa.