Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, Nasreddine Nabi amesema anatambua kwa sasa mahesabu yao ni kuhakikisha wanapata alama sita ili kutangaza ubingwa, lakini itawabidi wahakikishe wanapata ushindi katika mechi mbili zijazo ikiwemo ya Simba SC inayonolewa na Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ili kufikia malengo yao.

Nabi ametoa kauli hiyo licha ya Young Africans kukabiliwa na michezo miwili muhimu ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika ambapo keshokutwa Jumapili (Machi 19) wanatarajia kucheza dhidi ya Monastir kabla kuwafuata TP Mazembe katika mchezo utakaopigwa Aprili 02, mwaka huu nchini DR Congo kabla ya kurejea nchini kuwavaa Simba SC katika mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa Aprili 16, mwaka huu.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Young Africans inaongoza ligi ikiwa na alama 65 ikifuatiwa na Simba SC wanakamata nafasi ya pili wakiwa na alama 57 huku Singida Big Stars ikishika nafasi ya tatu na alama 48.

Nabi amesema anatambua ukubwa na ugumu wa michezo yao miwili ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika lakini haiwafanyi waache kupoteza malengo yao kwenye Ligi Kuu Bara kuelekea katika mchezo wao dhidi ya SC Simba kwa kuwa ni sehemu ya ubingwa wao msimu huu.

“Najua kwa sasa tunaangalia michezo hii miwili katika michuano ya kimataifa kwa sababu tunataka kuona tunaweza kufuzu hatua ya Robo Fainali kwa kuhakikisha matokeo makubwa yanapatikana kwenye mchezo wetu na Monastir ambao ndiyo utakuwa ni fainali kwetu ya kuweza kufikia malengo.”

“Lakini haiwezi kuondoka kile ambacho kipo mbele yetu hasa upande wa Ligi kwa sababu bado hatujashinda ubingwa na mchezo ujao utakuwa dhidi ya Simba SC, ambao wao watakuwa wakitaka kuona wanaweza kutufunga vipi, sisi tunaendelea kubadilika katika kila mchezo utakao kuwa mbele yetu kwa kuhakikisha matokeo yanapatikana,” amesema Nabi

Katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika Young African mpaka sasa wamefikisha alama 07 na kuendelea kubaki nafasi ya pili, huku US Monastir ikiongoza kwa kufikisha alama 10 na TP Mazembe ipo nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 03.

AS Real Bamako inaburuza Mkia wa Kundi hilo kwa kumiliki alama 02, baada ya kucheza michezo minne.

Rais Macron apitisha sheria ya kutatanisha maandamano yatanda
Ally Kamwe: Tumeshawasoma, tutawabamiza