Beki Kinda wa klabu ya Azam FC na timu ya taifa ya Tanzania U20, Pascal Msindo ameondoka nchini kwenda Uturuki kufanya majaribio ya mwezi mmoja katika klabu ya Antalyaspor inayoshiriki ligi kuu nchini Uturuki.
Hatua hiyo itamuwezesha Msindo kuzikaribia ndoto zake za kucheza soka la kuliowa barani Ulaya, kwani akifaulu atasajiliwa na klabu hiyo (Antalyaspor).
Kwa mantiki hiyo Msindo ataikosa michezo iliyobaki ya Kagame Cup inayoendelea kwa jijini Dar es salaam.
Azam FC leo itacheza mchezo wa pili wa kundi B dhidi ya Massager Ngozi ya Burundi, baada ya kuichapa KCCA ya Uganfa mabao 2-0 Jumatatu (Agosti 02).
Azam FC imekua chachu ya maendeleo ya soka kwa vijana na tayari imefanikiwa kutoa vijana (Wachezaji) wengi wanaotamba na waliotamba na timu za ndani na nje ya Tanzania.