Imebainika Mkoa wa Iringa kuna baadhi ya wananume wenye tabia ya kunyonya maziwa ya wake zao wanaonyonyesha, huku ikielezwa kuwa kitendo hicho ni mojawapo ya sababu zinazochangia tatizo la udumavu kwa watoto mkoani hapo, ambapo Iringa inashika nafasi ya tatu kitaifa.

Akizungumza na Dar24Media Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga amekili kuwepo kwa tatizo hilo, na kusema kuwa uongozi wa Mkoa umekuja na kampeni maalum kwaajili ya kuanzisha vikundi vya kinababa vitakavyoelimisha umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto, malezi, Afya pamoja na kupinga unyanyasaji wa kijinsia.

Aidha RC Sendiga amesema kuwa kitendo cha wanaume kunyonya maziwa badala ya watoto ni kitendo cha ukatili wa kiafya kwa mtoto, huku akielezea mkakati mwingine wa kupambana na jambo hilo ni kupitia kamati za lishe kutoa elimu kuanzia ngazi ya kifamilia, lakini pia kuweka wahudumu wa afya kuanzia ngazi ya chini.

Akizungumzia changamoto za udumavu RC Sendiga, amesema kama Mkoa wamekuja na kampeni ya kila kaya kulima mazao ya chakula pamoja na mazao ya biashara ili kuondokana na tatizo la udumavu.

Amesema kuwa wamefanya hivyo kwasababu wanaolima sana katika Mkoa wa Iringa ni watu wanaotoka nje ya mkoa huo na ndio maana inaoneka mkoa unarutuba ya kulima mazao yenye lishe lakini udumavu bado upo kwa kiasi kikubwa.

Aidha RC Sendiga amewahasa wazazi kuacha ulevi wa kupindukia unaopelekea kushinda muda mwingi kilabuni, pia amewasisitiza kuacha kuwapa watoto ulanzi wa sukari kitu ambacho sio afya kwa mtoto hasa katika ukuaji.

Pascal Msindo atimkia Uturuki
Haji Manara aendeleza vita mitandaoni