Mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia, Patcho Mwamba, ameweka wazi kwamba atakuja kivingine katika kuendeleza sanaa ya uigizaji ambayo inaonekana kudorora.
kwani wabongo bado wanapenda filamu za kibongo ila wanaishia kuangalia filamu za kinaigeria na kihindi zenye tafsiri ya kiswahili, wanaangalia hizi kwa kuwa sokoni hakuna kazi na amabazo zipo ni zile zenye ubora mbovu wa hadithi, picha, sauti na uigizaji.
Patcho alisema mwaka jana ulikuwa mbaya kwa wasanii lakini kwa mwaka 2017 amejiandaa kurudisha zama za Kanumba kwa kutoa Filamu zenye ujumbe na mvuto kwa mashabiki wake.
”Sisemi narudi vipi lakini nitarudi kwa kasi na namna nzuri ya kuwavuta mashabiki wangu na wa sanaa ya uigizaji kwani wengi wamepoteza matumaini, nataka kuwaahidi kwamba watafurahi na kazi nitakazokuja nazo mwaka huu hawatajilaumu tena kwa kukosa kazi kwa muda mrefu,”.
Fursa ipo kwa wasanii kuamka tena na kuliteka soko la ndani na Afrika kwa ujumla, mna haiba, mvuto, vipaji vya kuweza kufanya hivyo. Changamoto zipo katika kila kazi.
Kuweni wabunifu katika kazi zenu, mkianza kuwekeza nguvu katika kufanya yaliyo bora ni rahisi kutatua changamoto mlizonazo.
Mwaka huu uwe wa mabadiliko kwenu, oneni wivu kuona nyie ndo mnafanya kazi ya kupromote kazi za Bongo Flava na Bongo Flava hawana cha kusapoti kutoka kwenu. 2017 uwe mwaka wa mabadiliko kwenu na tuone mkiliteka soko kwa mara nyingine.