Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amekutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Rais wa Nigeria Profesa Ibrahim Gambari nyumbani kwake Chato Mkoani Geita, aidha mazungumzo yao yalilenga katika masuala mbalimbali ya uhusiano kati ya Tanzania na Nigeria.

Aidha, Rais Magufuli amempongeza Rais Muhammadu Buhari kwa jitihada kubwa anazochukua kwa ajili ya kuleta maendeleo nchini mwaka.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amempongeza Rais Buhari kwa jitihada anazozifanya za kukabiliana na kundi la Boko haramu ili kuhakikisha amani inaendelea kudumu nchini mwake.

Kwa upande wake Mjumbe Maalum wa Rais wa Nigeria, Profesa Ibrahim Gambari amempongeza Rais Magufuli kwa ushindi alioupata na jitihada anazochukua katika kupambana na rushwa na kubana matumizi jambo ambalo linaungwa mkono na wananchi wengi wa Nigeria.

Profesa Gambari amemkabidhi Rais Magufuli barua yenye ujumbe maalum kutoka kwa Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria

Patcho Mwamba: Nimejiandaa kurudisha zama za Kanumba katika Filamu
NEC yatoa onyo kali uchaguzi mdogo Dimani