Beki wa zamani wa klabu ya Manchester United Patrice Evra ametimuliwa katika klabu ya Marseille na amefungiwa kushiriki mashindano ya UEFA msimu huu baada ya kumpiga teke shabiki wa klabu hiyo ya Marseille.

Mchezaji huyo aliyewahi kucheza katika klabu za Monaco na Juventus amefungiwa na shirikisho hilo la soka Ulaya hadi Juni 2018, mwezi ambao mkataba wake na  Merseille ungemalizika huku akipigwa faini ya euro 10,000 (£8,829).

Evra alimpiga teke shabiki aliyekuwa karibu na uwanja kwa madai kuwa alimtukana kabla ya kuanza kwa mchezo wa Europa League, dhidi ya klabu ya Vitoria Guimaraes tarehe 2 Novemba.

Picha za video zinamuonesha mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United mwenye miaka 36 akiruka juu na kumpiga teke shabiki huyo ktendo kilichopelekea mchezaji huyo kufukuzwa uwanjani hata kabla ya mechi kuanza.

Patrick Evra

Gazeti la Ufaransa la L’Equipe limesema mashabiki wa Marseille walikuwa wamemzomea Evra kwa karibu nusu saa wachezaji walipokuwa wakijiandaa kwa mechi.

Evra alikuwa ameenda kuzungumza nao kuwatuliza lakini badala ya kupunguza kelele, wakazidisha na hali ikabadilika ghafla.

Olympique de Marseille fans hold a banner aimed at Evra, reading: 'You thought you were above the institution OM and its supporters. We don't want you wearing our colours.'

Mashabiki wa Marseille wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe kwa Evra ”Ulidhani uko juu ya sheria hatutaki kuona umevaa jezi yetu

Beki huyo wa Ufaransa alijiunga na Marseille Januari 2017 kutoka Juventus, klabu ambayo alikuwa ameichezea kwa misimu mitatu baada ya kuondoka Old Trafford.

 

 

Sadio Mane aipeleka Senegal kombe la dunia
Video: Mnada nyumba za Lugumi siri yafichuka, Wabunge CCM, Ukawa waibana Serikali