Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amefunguka kwamba, kuna watu wanatamani kuona wanatwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa na wengine hawapendi, huku akibainisha kwamba hajui kama anapata sapoti kutoka kwa timu za England.

Hii ni kuelekea Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo itapigwa keshokutwa Jumamosi (Juni 10) kati ya Man City dhidi ya Inter Milan, katika jiji la Istanbul nchini Uturuki.

Itakuwa ni fainali ya pili kwa Manchester City katika michuano hiyo wakiwa na Guardiola, baada ya ile 2020- 21 kupoteza dhidi ya Chelsea.

Guardiola amesema: “Kuna watu wanataka kuona Man City ikishinda UEFA, lakini wengine hawapendi, kuna baadhi ya klabu ni marafiki wanatamani kuona tukishinda, ila wengine ndiyo hivyo.

“Lakini jambo la msingi ni sisi kuwafunga Inter Milan bila kujali hayo yote.

“Najua sisi ndiyo tunapewa nafasi kuelekea mchezo huo, ni lazima tupambane. Ikifika fainali kama hii unakuwa na hofu bila kujali ubora wa wapinzani wako.

“Kuhusu kupata sapoti kutoka kwa timu za England na mashabiki wake kutusapoti sisi, hilo mimi sifahamu kama lipo.”

Ummy azindua Baraza jipya la Madaktari Tanganyika
Mama auwa watoto wake kwa kisu, amjeruhi mumewe