Ushirika wa ufadhili wa Kimataifa umesema Pete ya “mapinduzi” ya kuzuia HIV ambayo itavaliwa ukeni inatarajia kuzinduliwa hivi karibuni nchini Afrika Kusini, ambayo ina maambukizi mengi zaidi duniani,

Kupitia Mfuko wa Golobal Funds katika mapambano ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria, vikundi vitatu vinavyohusika katika mapambano dhidi ya UKIMWI nchini humo vinaunga mkono jitihada hizo, vimeweka oda ya awali ya pete 16,000 — ambazo zinatarajiwa kupatikana katika miezi ijayo.

“Tuna hakika kwamba pete hii mpya (pre-exposure prophylaxis) inaweza kuwa na matokeo ya kimapinduzi katika kuzuia VVU,” alisema Peter Sands Mkurugenzi mtendaji wa Global Fund.

Pete hiyo ya silicone, ambayo huvaliwa muda wote na kubadilishwa kila mwezi, hutoa dawa ya dapivirine inayorefusha maisha na utoaji wa awali utatumika kama hatua ya kwanza ya kuongeza upatikanaji wa matibabu na kuifanya ipatikane kwa urahisi katika nchi hiyo ambayo karibu watu milioni 8 wanaishi na VVU.

@Voa.

Gamondi ashindilia msumari Ligi ya Mabingwa
Simba, Young Africans zimeleta AFCON 2027