Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Malawi Peter Banda amerejea jijini Dar es salaam akitembelea Gongo, kufuatia majeraha alioyapata jana Jumatano (Novemba 09), wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Big Stars.
Banda aliyechukua nafasi ya Mkude kipindi cha pili, aliisaidia Simba SC kupata bao la kusawazisha kwa kutumia uwezo binafsi uliopelekea kufunga bao kwa ufundi mkubwa.
Kiungo huyo hakufanikiwa kumaliza salama mchezo huo, kufuatia rafu mbaya aliyofanyiwa na mchezaji wa Singida Big Stars, hali ambayo ilimlazimisha kupelekwa hospitali kwa ajili ya kufanyiwa matibabu na ndipo alipopatiwa msaada wa Gongo la kutembelea.
Kwa mazingira hayo Banda hatakuwa sehemu ya Kikosi cha Simba SC kinachoanza maandalizi ya Mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ihefu FC utakaopigwa Jumamosi (Novemba 12), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Banda alisajiliwa Simba SC mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Nyasa Big Bullet ya nchini kwao Malawi.