Mshambuliaji wa Simba SC Moses Phiri amesema kuwa sasa malengo yake ni ni kuhakikisha anapambana ili arejee katika kikosi cha kwanza cha Mbrazili, Roberto Oliviera.

Mshambuliaji huyo kutoka Zambia Jumapili (Agosti 20) alifunga bao lake la kwanza msimu huu wa Ligi Kuu Bara, timu hiyo ilipocheza dhidi ya Dodoma Jiji wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.

Nyota huyo katika msimu uliopita alipoteza nafasi katika kikosi cha kwanza kutokana na majeraha aliyoyapata katikati ya msimu uliopita.

Akizungumza jijini Dar es salaam Phiri amesema kuwa, anaamini jitihada alizoziweka katika msimu huu ni kupambana apate nafasi ya kucheza katika kikosi hicho cha kwanza cha timu hiyo.

Phiri amesema kuwa, icha ya ushindani uliokuwepo hivi sasa wa wachezaji wapya ambao wamesajiliwa, lakini hiyo haimfanyi yeye aingie katika kikosi cha kwanza katika msimu huu.

Ameongeza kuwa kwa sasa atakachokifanya ni kutumia vema katika kila nafasi atakayoipata kufunga na kuwatengenezea wachezaji wenzake ili wafanikishe malengo ya kubeba ubingwa wa ligi.

Kwa sasa malengo yangu ni kupambana, kila nitakapopata nafasi ya kucheza kwa kuonyesha ubora wangu wa kufunga mabao ili niingie katika kikosi cha kwanza.

Ninafahamu ushindani mkubwa uliokuwepo hivi sasa ndani ya timu, nitakachokifanya ni kutumia vema kila ninapopewa nafasi ya kucheza kwa kucheza kwa kujitoa ili nimshawishi kocha aendelee kuniamini.

“Haitakuwa kazi nyepesi kwangu bila ya kujibidiisha mazoezini kwa kuonyesha ubora wangu ili kocha anipe nafasi ya kucheza katika timu,” amesema Phiri.

John Stones kukosa Ligi Kuu
Majenerali Sudan wazidi kuwasha Moto, hali ni tete