Nahodha na Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi leo Jumatano (Januario 04), amerejea Paris kujiunga na Wachezaji wenzake wa Klabu Paris Saint-Germain, kwa ajili ya michezo ya Ligi ya Ufaransa.

Messi alikiongoza kikosi cha Argentina kutwaa Ubingwa wa Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar, na kuandika historia ya kuwa mchezaji Bora wa Fainali hizo ambazo zilifanyika kwa mara ya kwanza Mashariki ya Kati.

Wakati akiwasili Uwanja wa Mazoezi wa Paris Saint-Germain, Messi alipata mapokezi ya heshima, ambapo katika mapokezi hayo walimfanyia Gwaride la Heshima (Guard of Honour), ikiwa ni ishara ya kuthamini ya alichokifanya kwenye Fainali za Kombe la Dunia 2022.

Mkopo wa HELB kufutwa nchini Kenya
Nelson Okwa: Sijui lolote kuondoka Simba SC