Kikosi cha Namungo FC kimerejea jijini Dar es salaam kikitokea Kisiwani Unguja ‘Zanzibar’ kilipokuwa kikishiriki Michuano ya Kombe la Mapinduzi 2023.

Namungo FC ilicheza Nusu Fainali ya Pili ya Michuano hiyo jana Jumatatu (Januari 09), Uwanja wa Amaan dhidi ya wenyeji Mlandege FC.

Mchezo huo ulimaliza Dakika 90 kwa timu hizo kufungana 1-1, hali ambayo ilimlazimu Mwamuzi kutumia kanuni ya Mikwaju ya Penati, na Mlandege FC ilichomoza na Ushindi wa Mikwaju 5-4.

Namungo FC imerejea Dar es salaam na sasa inaelekeza nguvu zake kwenye maandalizi ya Mchezo wa Mzunguuko wa 20 wa Ligi Kuu dhidi ya Polisi Tanzania, utakaopigwa Januari 14 katika Uwanja wa Majaliwa mjini Ruangwa mkoani Lindi.

PICHA: Mo Dewji atinga kambini Dubai
Singida Big Stars na sintofahamu za Fancy Kazadi