Kikosi cha Simba SC kimeondoka jijini Dar es salaam leo Julai 23 jioni, na kuwasili salama mkoani Kigoma.
Simba SC imewasili mjini Kigoma saa kumi na mbili jioni, na kulakiwa na Mashabiki wa klabu hiyo walijikusanya Uwanja wa ndege kwa ajili ya kusubiri msafara wa timu yao.
Mapema leo asubuhi Young Africans iliwasili mjini Kigoma na kupata mapokezi makubwa kutoka Mashabiki wao.
Timu hizo zitakutana katika mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho *ASFC,* Jumapili (Julai 25) Uwanja wa Lake Tanganyika.