Azimio la pamoja, lililowasilishwa na Marekani kwa ushirikiano na Albania kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupinga kitendo cha Urusi kujitwalia maeneo ya Ukraine, limegonga mwamba baada ya Urusi kupinga kwa kutumia kura yake turufu.
Wanachama 10 kati ya 15 wa Baraza hilo waliunga mkono huku Gabon, ingawa China na Brazil walijiengua kwenye upigaji kura, ambapo Urusi na ambayo imetumia kura turufu au Veto ikafanya azimio lisiweze kusonga kokote, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiitaka Urusi isitekeleza mpango wake wa kutwaa maeneo ya Ukraine.
Akiwasilisha azimio hilo, Mwakilishi wa kudumu wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa, Balozi Linda Thomas-Greenfield, amesema huu si wakati wa kukaa kando, bali huu ni wakati wa kutetea Chata ya Umoja wa Mataifa kwa misingi na malengo yake.
Amesema, iwapo Urusi inachagua kujilinda yenyewe dhidi ya uwajibikaji, “basi tutapeleka hatua mbele kwenye Baraza Kuu ili kutuma Moscow, Urusi ujumbe usiotetereka ya kwamba dunia iko kwenye upande wa kutetea uhuru na eneo la mipaka.”
Balozi Thomas-Greenfield, pia amegusia kwamba dunia imeshuhudia Rais, Vladmir Putin wa Urusi akisherehekea ukiukwaji huu dhahiri wa sheria ya kimataifa kwa kuandaa hafla kujipongeza yeye nyuma ya kura ya maoni isiyo halali.
Akihutubia wajumbe, Balozi Vasily Nebenzya, ambaye ni Mwakilishi wa Kudumu wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa amesema kwamba nchi yake inalazimika kusema kuwa baadhi “ya wenzetu kwenye Baraza wamefikia kiwango cha chini na masalia ya utu kwenye ukumbi yamekiukwa.”