Rais wa Shirikisho la Soka Barani Ulaya UEFA, Michel Platini ameshindwa katika rufaa yake ya kupinga adhabu ya kufungiwa kwa siku 90 kujihusisha na masuala ya soka dunaini kote.

Platini, alikuwa amewasilisha rufaa akitaka marufuku ya kutojihusisha na soka kwa miezi mitatu iondolewe ili kumuwezesha kuendelea na kazi, lakini hilo limekataliwa na Mahakama ya Mizozo ya Michezo CAS.

Platini, mwenye umri wa miaka 60, alisimamishwa kazi pamoja na rais wa FIFA, Joseph Sepp Blatter mwezi Oktoba mwaka huu, huku uchunguzi wa madai ya rushwa dhidi yao yakiendelea kuchunguzwa.

Wote wawili wamekanusha tuhuma hizo.

Louis Van Gaal Ajipoza Kwa Kujipa Matarajio
Toure Kinara Wa Tuzo Ya BBC Afrika Mwaka 2015