Meneja kutoka nchini Argentina Mauricio Pochettino ameripotiwa atapenda kuwa na huduma ya Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane kama atakabidhiwa mikoba ya kukinoa kikosi cha Chelsea.

Kwa muda sasa Meneja huyo ambaye aliwahi kuvinoa vikosi vya Spurs na PSG amekuwa akihusishwa na kibarua cha kwenda kuinoa Chelsea kwa ajili ya msimu ujao.

Pochettino ameelezea mipango yake ya kuijenga timu ya Chelsea kwa vipaji matata kabisa, akiwamo Kane akimtaka akakipige Stamford Bridge ambako ndipo makao  makuu ya Chelsea yalipo huko Magharibi mwa jijini London.

Wakitarajia kutokuwa na soka la Ulaya msimu ujao, wakiwa na hasara ya Pauni 121 baada ya kutumia zaidi ya Pauni 600 milioni kwenye madirisha mawili ya usajili yaliyopita, Chelsea watahitaji kufanya mabadiliko makubwa kwenye dirisha lijalo.

Kuna mpango wa kupigwa bei mastaa kibao, ambapo kwa sasa Chelsea ina zaidi ya wachezaji 30, huku mchezaji wao katika anayecheza kwa mkopo Brighton & Hove Albion, Levi Colwill naye anaweza kurudi kuja kucheza kwenye kikosi cha Pochettino

Kwa msimu ujao, Chelsea itakuwa na huduma ya Mshambuliaji wa Ufaransa Christopher Nkunku, ambaye atakwenda kujiunga na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu akitokea RB Leipzig.

Kwa mujibu wa Daily Mail, Pochettino anatarajia kuwaambia mabosi wa Chelsea wahakikishe wananasa saini ya Kane.

Mkuu wa shule apiga ramli shuleni
Real Madrid kutinga kibabe Ujerumani