Kiungo wa Juventus, Paul Pogba amepata majeraha kwa mara nyingine baada ya ushindi wa mabao 2-0 katika mechi ya Serie A mwishoni mwa juma lililopita.
Kiungo huyo ambaye aliingia kipindi cha pili hakuendelea na mchezo baada ya kuumia huku Kocha wa Juventus Max Allegri akisisitiza: “Bado hatujui kitu, nadhani Pogba alihisi maumivu, tutaangalia vipimo vitaonyesha nini.”
Tangu aliporejea Juventus kutokea Manchester United, Pogba alishindwa kumaliza mechi kutokana majeraha ya mara kwa mara.
Anapokuwa fiti kiungo huyo ni mmoja kati ya wachezaji wenye vipaji vya kucheza soka na anakuwa na mchango mkubwa na timu inapokuwa katika kiwango bora.
Lakini kutokana na majeraha kumuandama kocha wake ameingiwa na hofu na kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa.
Sasa maswali yameibuka kuhusu afya ya kiungo huyo kutokana na majeraha yake ambayo yanaleta changamoto kwa mipango ya kocha.
Hali ya afya ya Pogba imeendelea kuwa jambo la dharura ambalo Allegri na Juventus wanapaswa kulishughulikia kwa tahadhari na uangalifu mkubwa.
Mwezi uliopita Allegri aliulizwa kuhusua afya ya Pogba akajibu: “Kwa sasa bado sifahamu, sijui atarudi lini, alifanya mazoezi na wenzake, tuwe na matumaini kuanzia Agosti 7 anaweza akaongeza juhudi na kuwa fiti asilimia 100.”
Baada ya kurejea Pogba alisumbuliwa majeraha ambayo yalimweka nje ya dimba kwa muda mrefu, iliyopelekea akakosa fainali za Kombe la Dunia Qatar kutokana majeraha hayo.