Kamanda wa zamani wa Jeshi la Nchi Kavu la Poland Jenerali Waldemar Skrzypczak amesema Warsaw inapaswa kudai eneo la Kaliningrad kutoka kwa Urusi ambayo ililitwaa tangu 1945.
Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Super Express, wakati akifanyiwa mahojiano Jenerali Skrzyczak amesema, “Inaweza kufaa kuuliza eneo hili la Kaliningrad, ambalo, kwa maoni yangu, ni sehemu ya eneo la Poland.”
Baada ya Ujerumani kushindwa katika Vita vya pili vya Dunia, eneo lake la Mashariki mwa Prussia liligawanywa kati ya Muungano wa Sovieti na Poland USS
Russia ilipata takriban theluthi moja ya ardhi ya eneo hilo, pamoja na jiji la Konigsberg inayojulikana kama Kaliningrad tangu wakati huo, ikianzisha mkoa wa kisasa wa Kaliningrad.
Baada ya kuanguka kwa Umoja wa Kisovyeti, eneo hilo lilibaki kuwa eneo la Urusi, linalopakana na Poland na Lithuania.