Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Katibu wake wa NEC Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole kimewataka viongozi wake wa ngazi zote kuisimamia serikali katika ngazi zote na kuhakikisha wanajishughulisha na kutatua shida za wananchi kwenye maeneo yao,
Ameyasema hayo katika kikao cha kuimarisha na kukijenga chama hicho kilichofanyika Mkoa wa Kilimanjaro na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali,
“Mwaka huu ni wa ujenzi wa chama, kukumbushana misingi ya CCM, kutazama madhaifu na umadhubuti wake katika maeneo yote. Wanachama na viongozi muelewe Katiba, kanuni, taratibu na miongozo ya chama na zaidi viongozi msikilize watu na mtatue shida zao. Kiongozi wa CCM soma na somo kubwa kabisa lipo kwa watu, kuwasikiliza, kuelewa shida zao na malalamiko yao, hakuna somo zuri kama hilo kutoka kwa watu,”amesema Polepole
Hata hivyo, Polepole amewasisitiza wajumbe walioweza kuhudhuria kikao hicho dhana ya CCM ambayo ni kuisimamia serikali katika kila nyanja.