Baada ya Muigizaji wa filamu, Wema Sepetu kutangaza kurudi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole amesema kuwa chama hicho hakina taarifa yoyote ya kurudi kwa msanii huyo.
Polepole amesema kuwa CCM ina utaratibu wa mwanachama kujiunga na chama hicho na kuongeza kuwa chama chao siyo daladala.
Amesema kuwa mtu anaweza kupanda na kushuka wakati wowote apendao, na kwamba CCM ina misingi, imani na masharti ya uanachama.
“Ni heri abaki huko huko Chadema au akaanzie kule ambako alichukulia kadi yetu, Kuijenga CCM mpya yenye kuheshimu nidhamu ya chama siyo kazi ndogo na inataka viongozi wenye unyenyekevu, watumishi na wanachama wavumilivu. CCM mpya itakuwa chungu kwa baadhi yetu lakini tamu kwa wengi wetu,”amesema Polepole
-
Nusu ya madiwani wa Mbowe wameomba kuhamia CCM- Polepole
-
Msigwa awashangaa wapinzani wao kushangilia ushindi
-
Wabunge Chadema wazidi kusota rumande
Hata hivyo, ameongeza kuwa habari za Muigizaji huyo kurudi ndani ya CCM amezipata taarifa mitandaoni kama jinsi watu wengine walivyozipata.