Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole, amesema kuwa nusu ya madiwani kwenye baraza la madiwani la Halmashauri ya Hai wameomba kuhamia CCM.

Ameyasema hayo wakati akitoa tathmini ya uchaguzi mdogo wa madiwani, uliofanyika Novemba 26 kwenye kata 43 ndani ya mikoa 19 nchini.

Amesema kuwa Madiwani hao kutoka jimbo hilo ambalo mbunge wake ni mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe waliomba kuhamia CCM wakati ambao viongozi wa CCM walipopita kufanya tathmini ya hali ya kisiasa jimboni hapo.

“Tulipita pale Hai kipindi fulani ambapo ndio Moyo wa Chama Kikuu cha upinzani na wakatuomba sana karibu nusu ya baraza la madiwani kwenye halmashauri wahamie CCM lakini tukaona si vizuri wote waondoke,” amesema Polepole.

Uhuru Kenyatta kuapishwa leo, Nairobi
Magazeti ya Tanzania leo Novemba 28, 2017