Katibu Uenezi  wa CCM, Humphrey Polepole ametoa kauli nzito iliyozua majadiliano kwa baadhi ya wagombea ubunge wa CCM huku wengine wakijenga hofu na kutochangia hoja kwa kauli hiyo.

Polepole alihojiwa na moja ya kituo cha Radio Dar es salaam, na kusema wanachama watakaotaka kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mkuu wa 2020, wanatakiwa kuwa wakazi wa eneo wanalotaka kuwakilisha.

Na ameeleza kuwa kwa sasa ni wabunge wachache wa CCM wanaoishi kwenye maeneo yao ya kibunge.

Hivyo mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe kupitia kaunti yake ya twitter amehoji ukweli wa kauli hiyo  amesema.

”Polepole kaka hii ya Times FM kuwa 2020 mbunge lazima awe anaishi jimboni kwake ni kauli yako comrade,’’.

Wabunge wengine wameshindwa kuzungumzia hoja hiyo na kudai kuwa hawajasikia rasmi tamko hilo kutoka kwa katibu uenezi.

Mbunge wa Songwe, Philip Mulugo amesema hayupo tayari kuzungumzia suala hilo

Amesema ‘’ sikusikia ilipozungumzwa kwa hiyo sitaelezea chochote,’’ amesema Mulugo.

Aidha Wabunge wengine waliunga mkono hoja hiyo na kusema kwa kufanya hivyo itasaidia kutokomeza rushwa na watu wasiojulikana ambao hununua kura za watu  kwa fedha na kuishia kufanya ufisadi

 

Video: Itazame 'Penthouse Floor' ya John Legend akiwa na Chance the Rapper
Marekani, Iran zatunishiana misuli