Polisi nchini Afrika Kusini imesema tayari wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kisa cha moto kwenye jengo la bunge hapo jana.
Msemaji wa polisi Thandi Mbambo amesema mtuhumiwa anayehusishwa na kisa hicho atafikishwa mahakamani wiki hii.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kwa upande wake amewaambia waandishi wa habari kwenye eneo la tukio kwamba mtuhumiwa huyo aliyekamatwa ndani ya jengo hilo la bunge bado anahojiwa.
Amesema tayari wamefungua kesi ya jinai na atafikishwa mahakamani siku ya Jumanne.
Lakini pia alisema mfumo wa maji wa eneo kulikoshika moto ulishindwa kufanya kazi.
Jengo hilo la kihistoria la bunge lilishika moto jana Jumapili na kuunguza kabisa eneo wanakokaa wabunge, hii ikiwa ni kulingana na msemaji wa bunge Moloto Mothapo.
Hata hivyo hapakua na ripoti ya majeruhi.