Askari wa Jeshi la Polisi kutoka chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) wamewafariji
mahabusu na wafungwa katika Gereza la Segerea lengo likiwa ni kutambua kundi hilo muhimu kwa taifa.

Mwenyekiti wa mtaandao wa Polisi wanawake Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP-Anitha Semwano amesema wanatambua umuhimu wa kundi hilo katika jamii, na kusema Jeshi la Polisi walitumia siku ya wanawake duniani kuwapa elimu ya ukalii wa kijinsia na namna ya kutoa taarifa za ukalii katika jamii.

Kwa upande wake Mrakibu wa Magereza SP Iyunge Saganda amesema mchango wa askari hao utakuwa msaada mkubwa kwa wafungwa hususani wafungwa kike ambapo ametoa wito majeshi na taasisi nyingine kuiga mfano mzuri wa Jeshi la Polisi kwa kumbuka makundi ya wahitaji.

Naye mwanafunzi wa kozi ya mkaguzi msadizi wa Polisi WP Gift Msowoya amesema wanatambua umuhimu wa kundi hilo mara watakapomaliza kifungo chao kwani wanamchango mkubwa katika ujenzi wa taifa.

Akiongea mara baada ya kutolea kwa msaada huo, Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam na Mlezi wa Mtaandao huo Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Dkt. Lazaro Mambosasa amewapongeza askari hao kwa moyo wa kipeke wa kujali makundi maaalum.

Kampuni ya Yutong kufungua Karakana nchini
Uanzishaji program za fursa: Mkurugenzi Geita aipongeza GGML