Kocha Msaidizi wa Polisi Tanzania, John Tamba amesema kuwa wanatambua ushindani uliopo kwenye Ligi Kuu Bara ni mkubwa watapambana ili washinde mechi zilizobaki ili kufufua matumaini ya kubaki katika Ligi hiyo.

Polisi Tanzania ikiwa imecheza mechi 28 imekusanya alama 25 ikiwa nafasi ya 15, Ruvu Shooting iliyo nafasi ya 16 tayari imeshashuka rasmi daraja.

Kocha Tamba ambaye ni msaidizi wa Mwinyi Zahera ameweka wazi kuwa mechi zilizobaki ni za maamuzi kwao jambo watakalochukulia umakini kupata ushindi.

“Tuna mechi mbili ambazo zimebaki mchezo wetu dhidi ya Mtibwa Sugar ambao tumepata alama tatu huo umeisha hivyo kwa sasa tunaanza maandalizi ya mechi zetu zijazo.

“Kikubwa ni kupata ushindi kwanza hapo tutakuwa na nafasi ya kuendelea kubaki kwenye ligi na tunajua ushindani ulivyo nasi tutaingia kwenye mechi hizo kwa ushindani mkubwa,” amesema kocha huyo

Mwishoni mwa juma hili Polisi Tanzania itakua mgeni wa Simba SC katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam katika mchezo wa Mzunguuko wa 29.

Watatu watimuliwa Mbeya City
Ujumbe wa Rais Dkt. Samia juu ya maisha ya Membe