Afara Suleiman, Babati – Manyara.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limetoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia kwa walimbwende 15 wa mikoa mbalimbali nchini, ambao wanatarajia kuwania taji la miss Tanzanite mkoani humo, akiwemo Mwanahabari wa Dar24 Media Eva Godwin.

Akizungumza na Warembo hao, Mkaguzi Msaidi wa Jeshi la Polisi, Celestin Mushi amesema lengo la kuwatembelea na kuwapatia Elimu hiyo, ni kuwaomba kuwa mabalozi katika jamii na Taifa Kwa ujumla.

Mwandishi wa Dar24 Media, Eva Godwin (kulia) Kushoto ni Mwakilishi kutoka Jeshi la Polisi.

Amesema, “kwa atakae bahatika kuchukua taji hilo, basi akaseme juu ya kupinga ukatili wa kijinsia na kingono ikiwa ni pamoja na kupinga Kwa jamii kujichukulia Sheria mkononi.”

Shindano hilo, linatarajiwa kufanyika Novemba 11, 2023 likiandaliwa na Natha’s Entertainment, washiriki tupo 15 kutokea miko mbalimbali Nchini, ambapo mshindi wa kwanza atakabidhiwa kitita cha Shilingi 1 Milioni.

PURA yafanya tafiti kubaini Mafuta, Gesi asilia
Mbeya ni kitovu cha amani, Biashara - DC Malisa