Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, ACP Hassan Omary amesema uchunguzi unaonesha kuwa Mtumishi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Merisiana Temu (42) mbali na kuuawa pia vipo viashiria vya wizi katika nyumba yake.
Kamanda Omary amesema, mtumishi huyo aliuawa Julai 17 majira ya saa 3:30 usiku na mwili ulikutwa sebuleni kwake mtaa wa Mamboya Manzese uliopo kata ya Mkwatani Wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro majira ya asubuhi ambapo Luninga, godoro na simu ya mkononi aliyokuwa akitumia havikuwepo.
Akiongelea tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Kisena Mabuba amesema,t aarifa za kuuawa kwa mtumishi huyo walizipata majira ya saa nne usiku Julai 17 mwaka huu baada siku hiyo kutoonekana kazini bila ruhusa na simu yake ikiwa haipatikani
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka amesema Serikali iko makini na vyombo vya ulinzi vinafanyakazi suala hilo, ili kuhakikisha wilaya hiyo inakuwa salama wakati wote. na kusisitiza kamati ya ulinzi na usalama kuendelea kuchunguza aliyehusika na tukio hilo.