Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Kamishna Msaidizi wa Polisi, Marco Chilya ametolea ufafanuzi kuhusiana na vifo vya Watoto wawili vilivyotokea huko Mtaa wa Sido Wilaya ya Nyasa kwa kulipukiwa na kitu kidhaniwacho kuwa ni bomu.

Akithibitisha tukio hilo, Kamanda Chilya amesema kuwa lilitokea Oktoba 1, 2023 Kitongoji cha Sido, Kata ya Sido Wilaya ya Nyasa ambapo watoto hao Victor Mapunda (12) Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kilosa na Onesmo Francis (4) wote wakazi wa Sido walifariki dunia kwa kulipukiwa na kitu kidhaniwacho kuwa bomu la kienyeji, ambalo walikuwa wakilichezea baada ya kuliokotA maeneo ya mwambao wa Ziwa Nyasa.

Aidha, Kamanda Chilya amesema baada ya tukio hilo kutokea wataalamu toka Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wataalam wa milipuko wa Jeshi la Wananchi Tanzania – JWTZ, wamefika eneo la tukio kwa uchunguzi zaidi huku akiwataka wazazi na walezi kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kuhakikisha Usalama wa watoto wao unaimarika.

Aidha, amewataka pia wananchi wanaoishi maeneo hayo kuwa watakapoona kitu ambacho kinautata kwao basi waweze kutoa taarifa kwa viongozi wao wa mitaa na Jeshi la Polisi, ili hatua zaidi zichukuliwe.

Waziri ataka usalama, ampa mkandarasi saa moja
Upungufu wa umeme Gridi ya Taifa ni Megawati 300-350