Jeshi la Polisi mjini Hong Kong limevamia ofisi za tovuti moja ya habari za mtandaoni inayounga mkono demokrasia baada ya kuwakamata watu sita kwa njama ya kuchapisha chapisho la uchochezi.
Hatua hii inaongeza visa vya ukandamizaji dhidi ya upinzani mjini humo kwa hivi karibuni.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Idhaa ya kiswahili (DW) limesema waliokamatwa wanahusishwa na kituo cha habari cha Stand News ambacho ni moja kati ya vituo vya habari vinavyounga mkono demokrasia mjini humo.
Itakumbukwa gazeti la Apple Daily ambalo pia lilikuwa likiunga mkono demokrasia pia liliacha kufanya kazi mapema mwaka huu kutokana na visa hivyo.
Waliokamatwa wanakabiliwa na kifungo cha hadi miaka miwili jela na faini ya hadi dola 640.
Polisi inasema kuwa zaidi ya maafisa wake 200 walihusika katika msako huo na kwamba walikuwa na kibali cha kukamata vifaa muhimu vya uandishi wa habari chini ya sheria ya usalama wa kitaifa iliyopitishwa mwaka jana.