Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amewaelekeza TARURA kuhakikisha wanashirikiana na Baraza la Madiwani katika kuchagua Barabara za kipaombele Cha Ujenzi na sio kujiamulia hao wenyewe.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa ufunguzi wa kikao Cha bodi ya Barabara ambapo amesema Madiwani Kama wawakilishi wa Wananchi ndio wanaelewa Barabara zenye changamoto kubwa na zinazotegemewa na Wananchi wengi hivyo Ni muhimu wakashirikishwa.

Aidha RC Makalla amewaelekeza TARURA na TANROAD kuhakikisha wanalinda Miundombinu ya Barabara zao hususani maeneo ya watembea kwa miguu yasivamiwe upya na Wafanyabiashara.

Hata hivyo amewataka Wakandarasi wanaotekeleza Miradi ya Barabara kukamilisha Ujenzi kwa wakati na kushirikiana na Wananchi na Serikali ya Mtaa wa eneo husika ili wajue Nini kinaendelea katika mtaa wao.

Pamoja na hayo RC Makalla ametaka TANROAD, TARURA na Wakandarasi kuenda sambamba na maono ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwafikishia Wananchi Maendeleo kwa wakati.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Disemba 30, 2021
Polisi yavamia kituo cha Habari Hong Kong