Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Ruhembe Mkoa wa Morogoro Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Kashorael Mnuo amewapa mbinu wakazi wa eneo la Kidodi Madukani, Kata ya Kidodi wilayani hapo juu ya namna ya kujilinda dhidi ya watu wanaofanya vitendo kinyume na sheria ikiwemo wizi wa mali na mifugo yao.

SSP Nunuo aliyasema hayo wakati alipokutana na wananchi wa eneo hilo kwa lengo la kuwaelimisha juu ya miradi ya Jeshi la Polisi ikiwemo kauli mbiu ya Ongea nao inayoendelea kutekelezwa maeno mbalimbali nchini.

Amesema, ushirikiano wa jamii na Jeshi la Polisi, hususan kupitia vikundi vya ulinzi shirikishi ni njia sahihi itakayosaidia kutanzua uhalifu katika mitaa kwa vile uhalifu unafanyika kwenye Jamii wanazoishi.

Kwa upande wake Polisi Kata wa Kata Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Aiden Mufundi ambaye aliambatana na OCD, alikumbusha wajibu wa kila mwananchi katika ulinzi wa eneo lake, huku akiwataka kutoa ushirikiano kwa vikundi vya ulinzi shirikishi, vilivyopo katika mitaa yao.

Muhubiri jela kwa kuchapisa maudhui bila kibali
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 2, 2023