Kocha mpya wa Tottenham Hotspur, Ange Postecoglou amesema atakuwa na mazungumzo na Mshambuliaji Harry Kane ili kufahamu anachotaka kukifanya, wakati nyota huyo akiwindwa na FC Bayern Munich.

Mabingwa hao wa Ujerumani, wameripotiwa kuweka mezani ofa mpya ya Pauni 70 milioni kwa ajili ya kumsajili Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29.

Nahodha huyo wa England, Kane, ambaye mkataba wake na Spurs unamalizika mwezi Juni mwakani, amefunga mabao 30 katika Ligi Kuu England msimu uliopita 2022/23.

“Kane ni miongoni mwa washambuliaji bora wa sasa duniani na ningependa kumuona akicheza hapa msimu ujao,”

“Nataka kujitambulisha kwa Harry, kumpa kile ambacho nawaza kukifanya hapa, nipate pia kile ambacho anakiwaza na kufanya kazi kwa pamoja kusaka mafanikio.” amesema Postecoglou

Gamondi aahidi makubwa Young Africans
Kitayosce FC (Tabora United) yapangua kikosi