Mkuu huyo wa kundi la mamluki la Wagner, Yevgeny Prigozhin, amevunja ukimya ikiwa ni siku mbili baada ya kuongoza uasi ulioshindwa akisema hakukusudia kuipindua serikali ya Moscow.
Katika tamko lake la kwanza alilolitoa kwa umma tangu alipoonekana usiku wa Jumamosi Juni 24, 2023 amesema aliviondoa vikosi vyake katika mji waliokuwa wameushikilia, na kwamba wapiganaji wake walisimamisha kampeni yao, ili kuepusha umwagikaji damu.
“Tulienda kama ishara ya kupinga na sio kupindua serikali ya nchi”, alisema mkuu huyo wa Wagner katika sauti ya dakika 11 iliyotolewa Jumatatu jioni kupitia mtandao wa Telegram.
Prigozhin anadai azma yao ilikuwa ni kushinikiza masuala waliyoyaibua kipindi cha nyuma, hususan matatizo makubwa ya usalama wa nchi.Rais Putin wa Urusi aonekana kwa mara ya kwanza tangu uasi wa Wagner
Ndani ya sauti hiyo, Prigozhin anasikika akisema alitaka kuzuia uharibifu wa wapiganaji mamluki wa Wagner na kulazimisha makamanda waliohujumu kampeni ya kijeshi ya Urusi nchini ukraine kuchukuliwa hatua za kisheria.