Watawala wa Sussex wamemaliza ziara yao ya siku kumi katika baadhi ya nchi za Afrika huku wakitangaza kufungua kesi dhidi ya gazeti moja la Uingereza la Sunday Mail kwa kuandika, kuingilia na kuchapisha kinyume cha sheria barua binafsi aliyomuandikia baba yake, Thomas Markle pamoja na kuendesha kampeni za kuchapisha taarifa za uongo na kumdhalilisha mke huyo wa mtawala wa Sussex.
Kupitia waraka alioutoa, mtawala huyo wa Sussex amesema, hatua hizo za kisheria zinafanyika kama majibu ya kudhibiti “propanda zinazoendelea dhidi ya mke wake”
“Mwitikio chanya” wa upashaji habari za wawili hao katika ziara yao Afrika imefichua “upendeleo wa wazi” wa “chombo hicho ambacho kimekuwa kikimdhalilisha [Meghan] karibia kila siku kwa kipindi cha miezi tisa”. amesema Prince Harry.
Jana mke wa mjukuu wa malkia wa Uingereza, Prince Harry, Meghan Markel wametangaza kufungua kesi dhidi ya gazeti hilo kwa madai ya kuchapisha taarifa ya barua yake binafsi aliyomuandikia baba yake, Thomas Markle kinyuma na sheria.
Msemaji wa Gazeti hilo amesema litasimama ‘kidete’ kujitetea dhidi ya kesi itayofunguliwa na wanafamilia hao wa kifalme na wapo tayari kujitetea mahakamani.