Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ametoa tahadhari kubwa kwa watu ambao bado wanaendelea kujihusisha na vitendo vya ujangili ndani ya hifadhi za taifa zote nchini.
Ameyasema hayo wakati wa mahafali ya 52 na maadhimisho ya miaka 51 ya Taasisi ya Taaluma ya wanyamapori ya Pasiasi iliyoko mkoani Mwanza, amesema kuwa wao kama Serikali wamejipanga kushinda ujangili huo.
“Natoa tahadhari kwa wale wanaojifanya majangili sasa watambue kuwa wakienda kuvamia hifadhi zetu za taifa, hawatarudi salama, watakutana na vijana waliopikwa kwa mbinu za kijeshi na wameiva kwaajili ya kazi hiyo,”amesema Prof. Maghembe
Aidha, ameongeza kuwa vijana wengi wanaomaliza katika vyuo wamefanikiwa kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya dola majangili wapatao 800 ambao wamekuwa wakijihusisha na shughuli hiyo.
-
Manispaa ya Ilala yapewa onyo kali, yatozwa milioni 25 kwa uchafuzi wa mazingira
-
Serikali yapunguza gharama za dawa, vifaa tiba na huduma za afya
Hata hivyo, kwa upande wake mkuu wa chuo hicho, Lowaeli Damalu amesema kuwa kutokana na mafunzo bora, maaadili na nidhamu wanayoitoa kwa wanafunzi wao ameiomba Serikali kuwapatia ajira wahitimu katika chuo hicho.