Manispaa ya Ilala imepewa onyo kali na kutozwa faini ya shilingi milioni 25 kwa uchafuzi wa mazingira katika Dampo la Pugu KInyamwezi ambalo limekuwa likisababisha adha kubwa kwa wananchi wanaoishi jirani na eneo hilo.

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kupitia Mkaguzi wa Mazingira wa kanda ya Mashariki. Jaffari Chimgege limeitoza faini Manispaa  ya jiji la Dar es Salaam kiasi hicho kwa kosa la uchafuzi wa Mazingira na kutohudumia Dampo hilo ipasavyo.

Aidha, Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina, ameitaka Halmashauri ya jiji kuja na mpango mkakati utakaoweza kuupunguzia mzigo dampo la Pugu ambalo kwa sasa linatumika kupokea takataka zote za Halmashauri za jiji la Dar es Salaam na kuonekana kuelemewa na mpango huo utakaowezesha kila manispaa kuwa na dampo lake.

“ Hakuna kitu nisichopenda katika utendaji wangu kama kuona taasisi za Serikali zikiwa za kwanza katika suala zima la uchafuzi wa mazingira, faini hiyo ya jiji mtailipa ndani ya siku 14, na kuhakikisha mnarekebisha matobo yote yanayolalamikiwa kupitisha maji na kupeleka katika makazi ya wananchi pamoja na kujenga mifereji ya maji ya mvua, na maji ya sumu yaende katika mkondo sahihi wa maji hatarishi na bila kusahau kuruhsu maji hayo baada ya kujiridhisha na vipimo vinavyotakiwa,”amesema Mpina

 

Hata hivyo, Manispaa ya Ilala imetenga kiasi cha fedha shilingi Bilioni moja za kitanzania kwa mwaka wa fedha ulioisha pamoja na kuzungumza na wadau wa maendeleo ikiwa ni mkakati madhubuti wa kuweza kuboresha Dampo hilo kinalotumika kwa kiasi kikubwa na manispaa zote za jiji la Dar es Salaam.

Picha: Mwili wa Shaban Dede wazikwa jijini Dar es salaam
Watatu washikiliwa kwa tuhuma za mauaji Tabora